1 Kings 7:40-45

40Pia akatengeneza masinia, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.

Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi zote katika Hekalu la Bwana kama vile Mfalme Sulemani alikuwa amemwagiza, yaani:


41 nguzo mbili;
mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo;
nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo;
42makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);
43vitako kumi pamoja na masinia yake kumi;
44ile Bahari ya chuma na yale mafahali kumi na wawili chini yake;

45 masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.

Vyombo hivi vyote ambavyo Huramu alimtengenezea Mfalme Sulemani kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyong’arishwa.
Copyright information for SwhKC